|
Post by Titchaz on Sept 3, 2012 11:31:19 GMT 3
|
|
|
Post by Titchaz on Sept 3, 2012 11:40:40 GMT 3
Mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Mpiganaji Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo.Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akiwa amejeruhiwa vibaya kwa risasi .
Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yalipigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini na kudai kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu magari kadhaa yameharibiwa huku watu kadhaa wakiwa wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi wa NIPASHE.
Habari zaidi zitawajia kadri zitakavyopatikana.
Mola aiweke roho yake mahali pema peponi - AMINA
|
|
|
Post by jakaswanga on Sept 3, 2012 20:55:20 GMT 3
Titchaz,
I wonder how Jakaya Kikwete slept that night. When your security forces do this kind of killing, you know there is, Shakespeare revisited, something very rotten at the heart of your republic.
This bestiality must be condemned. Then it must be understood. For it is a symptom of something. Something sinister.
|
|