Bw OO,
samahani kwa kutokua angani kwa sababu ambazo hazingeweza kuepukika. Kenya yetu kwa leo bado ina mshike mshike wa nguvu na hali halisi mpaka sasa haijaeleweka.Kabla sijaendelea ningependa kumjibu huyo
Nereah maana naona kana kwamba anamisemo isioeleweka.Kwa taarifa yake
neno ni taulo na sio taweli.Pia kuoga sio usafi bali ni mojapo tu ya njia za kuwa msafi.Kwa hivyo unaeza kuoga na ukawa mchafu bado.Kisha huu msemo nimejaribu kuona kama unahusika na mada inayojadiliwa lakini bado sioni vipi!
Kurudia mada husika ningependa kusema kwamba huyu Bw Kibaki na wapambe wake wa PNU wanazidi kutuhadaa na kuendekeza sera zao za kuganda mamlakani.Kwa kweli njia tulizobaki nazo kukabiliana na hawa watu lazima zitumike ipasavyo.Kwanza kabisa Kotini hatuendi na liwe liwalo.Kumbukeni sehemu yenyewe imeshehena vibaka wa MK na hamna haki na ukweli kutoka huko.Huyo Uhuru Kenyatta na Martha Karua inabidi wafunge midomo yao na waache kuwaambia wakenya maneno yasiokua na maana.
Kenyatta mwenyewe hajatuambia haya mashamba yaliopo hapa Pwani waliyapata vipi.Asishangae kuona wananchi wenye ari mpya wakitaka wapewe haki zao za kumiliki hizi sehemu.
Miaka zaidi ya arobaini imepita nasi bado maskwata tu huku mtu ana maelfu ya ekari tulionyanganywa sisi.Aibu ilioje hii na mtu anajaribu kutuambia eti anajali maslahi ya Wakenya!!Sidhani...anajali maslahi ya jamii yake.
Tunapofanya maandamano katika pembe zote za jamhuri, inaanza kuonekana wazi kua polisi wanaotumwa na serikali wanamwelekeo mmoja tu ambao ni
'ua na angamiza chochote kinachotembea'...hususan wajaluo.Sio siri!Tumejaribu kuwa na amani miongoni mwetu lakini tabia za hawa mwera zinaonyesha wazi kua wanataka kuua.Sasa hebu niambia kama atahukumiwa mtu baada ya hili vumbi kutulia.Kuna yule polisi aliyekamatwa na kamera za waandishi wa habari na kuonyeshwa kwenye runinga ulimwengu mzima.Haki ipo hapo kweli? Kutuibia kura wameiba,kutupiga wametupiga, kutupiga risasi wametupiga...kutuua wametuua na hata tukishakufa wanazidi kutupiga mateke.
Yaani unapiga mfu na huna hata aibu Hii kweli ni serikali ilioshehena mazimwi yanayofurahia damu ya wakenya wenzao ikimwagika. Ole wenu zamu ya mwenzenu ikifika na mgeuzwe nyie!!!!
Mtazamo mwengine ninaoomba ufanyike ni
usitishaji wa misaada na Jumuiya ya Mataifa ya Bara La Uropa na Benki ya Ulimwengu.Naona kama hawa jamaa watafanya kweli kulingana na kwamba hawakubali kamwe matokeo ya kura za mwaka jana.Kwa kufanya hivi watakua wanampa Kibaki onyo kubwa dhidi ya siku zake mamlakani.Nakuomba Bw. Onyango kama unaeza kukutana nao(maana naamini unaweza), waambie sio wasia mzuri(it is not prudent) kwa wao kusema eti Raila na Kibaki wakutane pamoja na kutafuta suluhisho la kudumu.
Kumbuka Kibaki ni mwizi, ni mwizi, ni mwizi na sio siri.Kibaki anachuki za wale wakikuyu wa zamani ambao walikua wanawachukia wajaluo kwa sababu Kenyatta said so.Ni mshamba kwa lugha nyepesi maana siamini kama anajua kulikoni katika Kenya ya Karne ya leo.Kwa hivyo sio sawa kumwambia Raila akae meza moja na mahluki kama huyu maana atakua anajimiksi na uozo mtupu.Si ni wao wamarekani na waingereza wanaosema eti
'we don't negotiate with terrorists'...hata kama Mmarekani yuko karibu kuawawa???Kwa hivyo sisi kama ODM
..."we do not negotiate with election thieves.Period!".How about that?Kibaki aturudishie ushindi wetu a'fu hayo mengine baadae.Iwapo jumuiya ya kimataifa itatuunga mkono basi nadhani kitaeleweka hivi punde.
Sehemu ya tatu ambayo inabidi tukabiliane na hawa vigunge ni Bungeni.Astaghafirulahi jamani!...mwenyezi Mungu si Athumani wala Onyango na hali Ugali...tumeshinda kiti cha Speaker oyeee! ;D Yaani walidhani pia hapa wataiba lakini wapi!Wakadhani watawahonga wabunge waODM lakini wapi!Wakadhani tutafarakana wenyewe kwa wenyewe lakini wapi!Imara daima tutasimama!Pale Bungeni kutakua na seketa la nguvu na kama tulivyoona juzi Mh. Orengo na Mh. Tawfiq wakimpa MK mavituzzz ya nguvu.
Kiraitu alipojaribu kuongea ilibidi atolewe ushamba na Mh. Orengo.Fanaleki jamani.Hivi ndivyo Bunge linavyotakikana kua...wanaume kwa wanawake wakijadili midahalo ya nguvu.PNU chuma chenu kiko motoni na nadhani hakuna mtu upande wao anayeweza kutukabili kwenye midahalo isipokua
Kabando wa Kabando( naye sidhani kama ni PNU vile.Kumbuka alisema kua jamaa walihongwa na kutishiwa jamii zao.Iko kazi hapo).Heri ya Kibaki labda ni afunge Bunge na asidhubutu kulifingua kamwe na sidhani anataka kufanya hivyo.
Serikali itakua inaendeshwa na vitengo viwili tu..Executive na Judiciary...taswira ambayo hatotaka kuonyesha Ulimwengu mzima.Lakini tena si unajua Kibaki alikamatwa na homa ya baridi na mwelekeo wake katika maswala nyeti hauaminiki.Basically he can do anything maana hana soni kama mtoto wa kelbu.
Kwa kutamatisha nduguzanguni wakenya, tusichoke kumkabidhi huyu mahluki aliyeganda kitini kama mfalme Binta....anayeishi katika nchi za Kufikirika na Kusadikika.Hii ni Kenya yetu ya leo na mola katunusuru il'mradi tuishi raha m'starehe kwa amani.Wezi kama Kibaki na wauaji kama Michuki watakiona cha mtema kuni arobaini yao ikifika.
Kwa mara nyengine tena, asante Bw. OO kwa kutuwezesha kubadilishana mawazo katika hii tovuti yako.Heshima yako kaka.Naomba kuwasilisha.
Ndimi wako mwaminifu,
Ab-Titchaz wa Kisauni,MombasaP.S. Bw OO, tafadhali nipe taarifa kuhusu msimamo wa
Mh Githunguri na ODM. Nilikuwa na wasiwasi mkubwa kwamba atatuwacha lakini bado amesimama.Mufti sana hio!!!