Post by Onyango Oloo on Apr 15, 2015 18:10:02 GMT 3
As someone who participated in the planning and convening of the April 14, 2015 press conference to denounce the draconian steps against
Haki Africa and
MUHURI
(I wrote and delivered the Kiswahili version of the media release) I may be accused by some to have a certain bias-which I readily own up to.
In my view, our event was a success because among other things:
(a) We invited the media and they showed up;
(b) We delivered our media release;
(c) Several representatives of various media houses-CCTV; KTN; NTV; AFP;Reuters, GBS, engaged us with tough questions to which we gave candid answers;
(d) We succeeded in dispelling the myths, gossip, innuendoes and plain falsehoods used by the Jubilee regime to tarnish the names of MUHURI and Haki Africa in linking them with terrorists;
(e) We acted in solidarity with the 600,000 refugees at Dadaab Camp that the government want to illegally close in total violation of Kenyan, African Union and United Nations laws, statutes, conventions and international obligations;
(f) We strengthened our unity and solidarity as human rights organizations-local, regional, national and international- by rallying in a timely manner, to our two sister CSO partners at the Coast;
(g) We set up several follow up interviews with the print and electronic media present;
(i) After our press conference, we left the Kenyan public better informed about the odious propaganda onslaught by the government against legal, peaceful and law abiding citizens and institutions wrongly tarred by the Al Shabaab terrorist slur simply they happen to be Muslim;
Here is a collage of snippets from the television stations which covered the event:
The English version of the press statement is available at this FIDH link.
Here is the Kiswahili version which Onyango Oloo translated from the original and presented at the press conference:
TAARIFA YA WAKEREKETWA KWA WANAHABARI
TAREHE KUMI NA NNE MWEZI WA NNE, NAIROBI
Kwanza kabisa twataka kuwasilisha rambi rambi zetu kwa wale wote walioathiriwa na tukio la ugaidi huko Garissa hivi majuzi.
Mkono wa tanzia kwa jamii, jamaa na marafiki wa vijana-wake kwa waume-mia moja arobaini na saba waliopoteza maisha baada ya kuuliwa kwa ukatili na wahalifu magaidi. Pole zetu kwa waathiriwa, waliojeruhiwa na manusura.
Wakenya tuwe watulivu, Wakenya tuwe wakakamavu; Wakenya, tushikamane kwa umoja amani na upendo.
Sisi Wakenya wakereketwa na vyama vetu vya kutetea haki za kibinadamu; sisi wanaharakati wa haki, sheria, Katiba na usawa, tumehuzunishwa, tumekasirishwa na kughadhabishwa na tukio haramu la kufungia ndugu na dada zetu MUHURI na Haki Africa walioko Pwani akaunti zao na kuwazuia kazi yao muhimu; shughuli zao halali na harakati zao za amani kupigia debe haki, usawa na maendeleo nchini.
Kulingana na ilani iliochapishwa katika jarida la Kenya Gazette, toleo la tarehe saba mwezi wa nne mwaka huu, Bwana Boinett anaesimamia idara ya Polisi ameodhoresha makundi matano akiyataja kama ya ugaidi zikiwa Al-Shabaab, Al-Qaida, MRC, ISIS na Boko Haram.
Ilani hiyo pia ina majina themanini na tano ambayo yana shukiwa kuwa na uhusiano wa karibu na Al-Shabaab. Orodha hilo inajumuisha makampuni, vikundi vya kufanya biashara, pamoja na watu binafsi. Ni ndani ya orodha hii ndio tumeshangazwa kuona majina ya vikundi vya kutetea haki MUHURI na Haki Africa.
Sisi wakereketwa tulio katika mstari wa mbele katika harakati za kutetea haki, maendeleo na usawa, tumefanya kazi kwa dhati, dhamira na ukakamavu na ndugu na dada zetu waliomo MUHURI na Haki Africa katika jitihada zetu usiku na mchana kuhamasisha Wakenya, hususan vijana kupinga itikadi kali zinazo nuia kutumia silaha na mabavu ili kuendesha kasumba ya ugaidi miongoni mwetu kote nchini na san asana katika sehemu za Pwani ufuoni.
Muhuri na Haki Africa ni vikundi halali vilivyosajaliwa na serikali. Shughuli zao ambazo ni za amani zinaendesha hadharani kwa njia ya uwazi na sheria.Muhuri na Haki Africa zinatambuliwa na kuheshimiwa sio hapa nchini tu bali kote ulimwenguni. Juzi juzi tu, Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Africa, ndugu yetu Hussein Khalid, alialikwa rasmi na Raisi wa Amerika, Mheshimiwa Barack Obama kushiriki kikamilifu katika kongamano ya kudadisi mbinu za kukabiliana na kupambania na ugaidi, kikao kilichoandaliwa sio kwingine bali ndani ya Ikulu sio hapa Nairobi lakini huku Washington DC kwenyewe.
Je, Amerika ambayo ina uzoefu mkubwa wa kumulika magaidi duniani wangesubutu kumualika Hussein Khalid kama wangekuwa wanamshuku kama mhalifu ama wangekuwa na shauku kuhusu msimamo wake ?
Wafadhili wa MUHURI ni pamoja balozi na serikali za kimagharibi ambao hawawezi kamwe kufananishwa na serikali yetu inayolegea na kuyumba yumba kwa wa upande wa kuwamulika magaidi darubini ya udadisi na uchunguzi..
Ndio maana tumepigwa na butwaa, tumewachwa vinywa wazi tukishangaa ni uwendazimu gani , ni kichaa gani ilisababisha MUHURI na Haki Africa ku orodheshwa na Al Shabaab, Al Qaeda na ISIS?
Ama ni kwa vile Hussein Khalid ni mwislamu na urefu wa MUHURI ni Muslims for Human Rights?
Imefika kiwango ambacho serikali ya Kenya itafanya Muislamu na Waislamu wasingiziwe ugaidi, uhaini na uhalifu kwa sababu tu ya dini yao?
Porojo na dhana hii potofu ni uwongo mtupu na inakiuka maadili, falsafa na sera za Katiba yetu.
Sisi wakereketwa tumekataa kata kata propaganda hii ya kuwagawanya na kuwagongoanisha Wakenya kwa misingi za dini, kabila, majimbo na hata rangi ya ngozi na aina ya nywele.
Kwa ufupi, Bwana Boinett hakufuata sheria alipochapisha ilani lake katika jarida la Kenya Gazette.
.
Sote twapinga ugaidi. Sote tuko pamoja na Wakenya wenzetu kupambana na Al Shabaab Al Qaeda na wahalifu wote wanaohatarisha amani na Usalama Kenya.
Lakini hatufungwa macho na porojo potofu ya wanasiasa wanaotaka kutuhadaa na kutugawanya.
twataka kumwambia Naibu wa Raisi Ruto wazi wazi leo kwamba ni kinyume ya sheria za Kenya; kinyume ya mikataba ya Umoja ya Afrika na maagizo za Umoja wa Mataifa kufunga kambi za wakimbizi nchini .
Twamsihi Bwana Ruto akumbuke Babake Raisi Uhuru, marehemu mwendazake Mzee Jomo Kenyatta hapo zamani za kale alikuwa mkimbizi huko ulaya kwa miaka takriban kumi na nane; twambia Bwana Ruto kwamba rafiki wa Jubilee Yoweri Museveni pia alijificha hapa Kenya kama mkimbizi; rafiki yao mwingine, Paul Kagame alilelewa Uganda kama mkimbizi kutoka Rwanda.
Wakubwa wa serikali wasidharau wakimbizi. Kwa bahati mbaya, siku za usoni kuna uwezekano kwamba baadhi yao waneweza kukimbilia hizo hizo kambi za wakimbizi zinazo simamiwa na UNHCR.
KUMALIZIA, TWADAI HAKI ZETU:
1. Kwanza kabisa, serikali ya Kenya ifanye hala hala, le oleo iondoe mara moja kutoka kwa orodha ya makundi za kigaidi;
2. Pili, serikali iaangazie kipengele arobaini na saba ya Katiba yetu kabla ya kuchukua hatua haramu na kinyume ya sheria;
3. Tatu, serikali ikome kabisa kuwabagua Waislamu, hususan Wasomali, Waswahili na Wakenya wenye asili ya Kiarabu;
4. Nne, serikali idumishe wajibu wake wakulinda Wakenya wote popote walipo; ili kuimarisha usalama, amani, umoja na maendeleo kote nchini. Suluhu wa kudumu kumaliza ugaidi na ukosefu wa usalama nchini itapatakina wakati serikali itaweka maana mizizi na chanzo za shida zetu ikiwemo tofauti za kitabaka, ukosefu wa kazi, umaskini nna ukabila;
5. Mwisho, Serikali ikubali na kushukuru kwamba vyama vya kijamii, vyama visivyo va serikali, na ndio vikundi vya kupigia debe haki za kibinadamu kama MUHURI, kama Haki Africa, zimechangia pakubwa mno kusukuma mbele gurudumu la maendeleo, amani, haki na usawa hapa kwetu Kenya. Badala ya kuzikashifu na kuziharibia jina kwa kuziorodhesha na al Shabaab, serikali yetu ni lazima itupe tuzo na zawadi kwa harakati zetu za kutoa Kenya kutoka minyororo za ufashisti na udikteta mpaka leo tuliomulikwa na nuru ya Katiba mpya.
6. Achilia MUHURI iwe huru!
Uhuru kwa Haki Africa!
SIGNED
14TH APRIL 2015
1. ……………………………………………
Kenya Human Rights Commission (KHRC)
2. …………………………………………..
The Kenya Section of International Commission of Jurists (ICJ Kenya)
3. …………………………………………..
National Coalition of Human Rights Defenders (NCHRD)
4. ………………………………………….
Kenyans for Peace with Truth and Justice (KPTJ)
5. ………………………………………….
Constitution & Reform Education Consortium (CRECO)
6. ………………………………………….
ARTICLE 19 Eastern Africa
7. ………………………………………….
Human Rights Watch
8. ………………………………………….
Freedom House
9. …………………………………………..
Mazingira Institute
10. …………………………………………...
UHAI - the East African Sexual Health and Rights Initiative
11. Lorna Dias, Executive Coordinator……..
Gay and Lesbian Coalition of Kenya, the (GALCK)
12. ……………………………………………
Commonwealth Human Rights Initiative (CHRI)
13. …………………………………………….
FIDH, within the framework of the Observatory for the Protection of Human Rights Defenders
14. …………………………………
OMCT, within the framework of the Observatory for the Protection of Human Rights Defenders
15…………………………………
Coalition for Constitution Implementation
14th April 2015.